mama Maria Nyerere
Mama
MARIA NYERERE ambaye ni mke wa baba wa taifa hili mwalimu NYERERE akizungumza
na wanahabari leo nyumbani kwake jijini DAR ES SALAAM
|
SAKATA la Ufisadi
wa zaidi ya Bilioni 400 kwenye Akaunti Tegeta Escrow iliyoko Benki kuu,lazidi
kuwaibua watu mbalimbali Kupinga wizi huo ,baada ya leo Mama Maria
Nyerere kuibuka na kuzivaa mahakama pamoja na Bunge kwa kitendo chake cha
kutumia kipengele cha sheria walizotunga wao kuwalinda wezi wanaliibia taifa
mabilioni ya mapesa.
Kauli hiyo ya mama Maria Nyerere ameitoa mda huu jijini Dar Es
Salaam,wakati alipokuwa anazungumza na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali
nchini kutaka kufahamu kuhusu mwenendo wa nchi,ambapo Mama Nyerere alisema
inashangaza sana viongozi wa leo ambao wanashindwa kumuenzi baba wa taifa kwa
kuzidisha wizi wa mali za umma huku wakilindwa na sheria walizozitunga.
“Yaani
inasikitisha sana leo watu wanasogeza mali za umma kwenda kwenye mifuko yao
huku tukishuhudia wengine hawana dawa kwenye hospitali,harafu tunaambiwa wezi
hawa wanaofanya unyama huu wanalindwa na sheria,wakati leo unapita kwenye mitaa
huku unamkuta mwizi ameiba kuku anachomwa moto,halafu anayeiba mali za umma
analindwa na sheria sasa hii sheria ikoje jamani kwa sababu wtu wanakufa kwa
kukosa dawa sheria haiwalindi hii ni vipi “ alihoji Mama Nyerere
Mama Nyerere alizidi kuongea kwa uchungu huku akitaka hata kulia
alisema kwa sasa Viongozi wamekosa maadili na kujikita kwenye wizi
wa mali za umma kutokana na mifumo ya kimaadili ambayo imeanzia kwenye Familia
na kupelekea hadi kwa watendaji wa serikali.
Kuhusu Katiba iliyopendekezwa
Mama nyerere alisema katiba ni jambo jema
katika nchi yeyote na akashanga kusikia leo watanzania wanagawanyika kisa
katiba.
“katiba ni njia nzuri ya kulijenga taifa na
tumeona hata nchi za Marekani wameifanyia marekebisho katiba zaidi ya mala
70,inakuwaje sisi leo katiba hii ndio itugawe kiasi hichi,leo katiba ndio
itupeleke kwenye hali ya kupoteza umoja wetu,kiukweli nawaomba viongozi wa
vyama vyote vya siasa watoe tofauti zote kwenye jambo hili la
katiba”alisema Mama maria Nyelele.
Vyombo Vya Habari
Mama huyo wa Mwasisi wa Taifa hili
akusita kuvionya vyombo vya habari nchini na kuvitaka viache kutumia
misamiati mibaya wakati wa kuripoti taarifa kwa wananchi na kuvitaka vitoe
taarifa na misamiati ambayo kuundoa misuguano kwa jamii kwani itaweza
kuwapunguzia hali ya ufanyaji kazi viongozi wa taifa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni