Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Jumatano, 10 Desemba 2014

ASHINDWA KUJIZUA KULA 'TISHU'


Jade anasema alinza kula karatasi alipokuwa na mimba yake ya mwsho lakini hadi leo hajaweza kukoma


Mama mwenye watoto watano, ameelezea kuwa yeye hula roli moja ya karatasi ya msalani au Tissue kila siku.
Jade Sylvester,mwenye umri wa miaka 25, alianza kutamani kula karatasi hio alipokuwa mjamzito lakini hata baada ya kujifungua yeye hujipata akila roli moja ya tissue kila siku.
Kwa mujibu wa jarida la Mirror, Uingereza, kwa mara ya kwanza alipata hamu ya kula karatasi hio ni pale alipokua na mimba ya mtoto wake mdogo Jaxon.
Jade, anayetoka mtaa wa Gainsborough, Lincolnshire, alinukuliwa akisema, "miezi mwili tangu kushika mimba hio, nilianza kutamani kula karatasi ya chooni. Hadi sasa sijui kwa nini mimi bado huila. ''
"ninapenda tu ninavyojisikia nikiiweka mdomoni mwangu, lakini sipendi ladha yake. Familia yangu huniambia sio visuri kwangu kuila , lakini siwezi kujizuia. ''
 
 Jade ni mama mwenye watoto watano na anasema ameshindwa kabisa kuacha uraibu wake wa kula karatasi ya msalanai
Licha yakujifungua mwanawe miezi 15 iliyopita, Jade hawezi kabisa kujizuia kutokula karatasi hio.
Mama huyo ambaye hafanyi kazi, anasema yeye husubiri anapopata haja kwenda chooni na hapo ndipo haunza kuila karatasi ile. Yeye huitafuna na kuimeza yote kila siku.
Amepata wakati mgumu kujaribu kukomesha uraibu wake tangu alipojifungua lakini anasema ameshindwa kabisa.
''Najua kwamba sio vyema kwa afya yangu, lakini hadi sasa sijapata matatizo yoyote ya kiafya kama wanavyohofia watu wengi.''
Jade ana watoto watano , wavulana wanne na msichana mmoja.
Anasema yeye hujaribu kujificha kutoka kwa wanawe kwa sababu anahofia wakimpata akila karatasi hio watamkanya sana.
chanzo bbc.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni