Diamond.
Nyota wa muziki Diamond Platnumz ambaye mwishoni mwa wiki ameweza kushinda tuzo tatu huko Afrika Kusini, amekuwa ni moja kati ya wasanii wakubwa Afrika walioshiriki katika project ya pamoja inayokwenda kwa jina We are the World Africa.
Kazi hii kubwa imefanyika huko Afrika Kusini ikiwashirikisha pia mastaa kutoka nchi nyingine za Afrika kama vile Banky W, Mafikizolo, Iyanya, Don jazzy na wengineo wengi.
Kabla ya kuondoka Tanzania Diamond aliiambia eNewz juu ya ushiriki
wake katika project hiyo kubwa, ikiwa pia na lengo la kuongeza uelewa
juu ya Gonjwa la Ebola ambalo limekuwa tishio nchi za Afrika Magharibi
na Afrika kwa ujumla.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni