Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Jumatatu, 15 Desemba 2014

SOMO LIPO TAYARI;-MADHARA YA KUFANYA MAPENZI KINYUME CHA MAUMBILE



Leo tunageuza shilingi upande wa pili kuelezea madhara ya kuruka ukuta (kufanya ngono kinyume cha maumbile), baada ya kuona madhara ya wanawake kurukwa  na nini kifanyike.
Wanaume wengi walinilaumu na kuniona sitendi haki kwa kuwaelezea wanawake tu wakati mchezo huwa una athari kwa mtenda na mtendewa.
Kama nilivyoelezea kwenye mada za wiki kadhaa zilizopita, mchezo huu unatumika sana katika mapenzi ya sasa, watoto wa mjini wana usemi wao kwa kitu kilichovuma kuwa ‘ndiyo habari ya mjini’.
Mchezo huu umekuwa ukipendwa sana na wanaume wengi ambao wengi wao huwa hawatumii kinga na kusababisha wengi kupata magonjwa ya zinaa pamoja na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU).
Lakini mchezo wa kuruka ukuta umekuwa na madhara makubwa sana kwa wanaume wanaoufanya kwa muda mrefu.
Tulipoangalia upande wa wanawake, tuliona sehemu kubwa ya wanaopenda mchezo huu ni wanaume ambao wengine wamebatizwa majina ya ‘basha’, wakimaanisha mwanaume mpenda kuruka ukuta bila kuangalia ni wa mwanaume mwenzake au wa mwanamke.
Kwa vile nia ya kona hii ni kuelimisha madhara ya mtu kupenda kuruka ukuta ili aache mara moja, tunaendelea kutoa elimu ya bure ili mtu yakimkuta ajue yamempata kwa kiburi chake na kwa kupenda starehe ya kipuuzi.
Madhara anayoyapata mwanaume anayependa mchezo huo ni kama ifuatavyo:
Kwanza: Husababisha kusinyaa au kuweka makovu kwenye njia ya haja ndogo.
Pili: Njia ya haja ndogo kuziba kiasi au kuziba kabisa.
Tatu: Kupata saratani (kansa) ya tezi za figo (prostate gland).
Nne: Kupata magonjwa sugu ya uti wa mgongo.
Tano: Kuharisha.
Sita: Maambukizi ya VVU ambapo mwisho wake ni Upungufu wa Kinga Mwilini (Ukimwi).
Saba: Baadaye mhusika kupata msongo wa mawazo au sonona kwa kujutia tendo hilo.Nina imani ndugu yangu umeona madhara mabaya sana ya tabia hiyo mbaya. Inawezekana umezoea mchezo huo wa kuwaingilia wenzako na kuona raha lakini tumeona madhara yake, ambayo kwa hakika kama wewe ni mmoja wao, unatakiwa kuacha mara moja kwa vile mwisho wake ni majuto na mateso.
Jiepushe kuiga mambo bila kujua faida na hasara zake pia usimtie mwenzako majaribuni kwa kumlazimisha kuingia kwenye mchezo huo. Wanawake wengi wamekuwa wakilazimishwa na wanaume kuingiliwa kinyume na maumbile kwa kuwatishia kuwaacha kama watakataa. Swali linakuja, kipi bora, kuharibiwa au kuachana?
Kumbuka baada ya kuharibikiwa, thamani yako hushuka na sifa yako ikiwafikia waharibifu wa watu, basi unageuzwa jamvi la mtaa na hatimaye unakufa kwa msongo wa mawazo au mateso ya ugonjwa utakaupata baada ya kukubali kuingiliwa kinyume na maumbile.
Unaweza kushangaa baada ya kuelezea madhara yanayowapata wanaume nimehamia kwa wanawake. Ukweli mchezo huu umewaathiri sana wanawake.

MC.RAY
WHATSAPP 0659/375263
INSTAGRAM MC.RAYMONDMUSHI
FACE BOOK Raymond Mushi
PAGE Rayshughuli


 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni