Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Jumanne, 9 Desemba 2014

NGONOYA MDOMO NI HATARI


kansa





Utafiti unaonyesha watu wengi hasa vijana wanamejiingiza kwenye vitendo hivi vya kufanya ngono wakitumia midomo hasa ndimi, hivyo kuhatarisha uhai wao.
Utafiti unabainisha kuwa asilimia kubwa ya vijana wenye umri kati ya miaka 20 hadi 45 wanatumia staili ya kuwanyonya wenza wao sehemu za siri lengo likiwa ni kuwavutia wapenzi wao katika kushiriki ngono.
Vijana wenye umri huo ndio wahanga wakubwa kwa sasa kutokana na ugonjwa huo kuonekana kuwaathiri kwa kasi, huku wengi wakiwa hawajui athari zake. Baadhi hujisifia kwamba ni wajuzi, kumbe wanajitafutia kifo kwa kufanya vitendo hivyo.
Utafiti unaonyesha kwa watu wazima walio wengi hawana muda wa kufanya hayo wanayofanya vijana, hivyo kujikuta angalau wanakuwa salama na kupatwa na saratani ya koo kwa njia hiyo inayoonekana kama ni chafu pia.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk Crispin Kahesa anasema saratani ya koo ni ya pili katika mtiririko wa saratani zinazowapata wanaume nchini, ikiongozwa na ile ya ngozi (Karposi’s Sarcoma) ambayo huambukizwa kwa njia ya kujamiana. Kuna saratani aina zaidi ya 24 zinazoisumbua Tanzania.
Anasema mbali na staili hiyo pia, kuna baadhi ya watu hupata saratani ya koo kwa kurithi kutoka kwa wazazi wao na wengine kuwa na umri mkubwa ambao huchangia kupata tatizo hilo, lakini siyo kwa asilimia kubwa kama ile ya ngono ya mgomo.
“Hali hii ya vijana wenye umri huo kuwanyonya wanawake inatokana na ujana, wengine wanaiga kwenye mitandao, lakini mambo haya hayakuwepo zamani tofauti na sasa, utakuta wanaume ili aweze kumvutia mwanamke anamfanyia hivyo sehemu za siri, lakini zamani staili hii haikuwepo kabisa,” anasema Dk Kahesa na kuongeza.
“Kuna njia nyingi tu za kumvutia mwanamke lakini siyo hii bila kujua madhara yaliyopo, vijana wengi nchini wanaona njia rahisi ya kupendwa na mwanamke ni hiyo wakati kuna njia nyingi za kufanya. Nje ya hiyo wanawake wengine huwa na magonjwa mbalimbali, kwa jumla hakuna usalama wowote kwa wanaume kufanya kitendo hicho,”anaongeza
Sababu nyingine zaidi
Anasema staili ya maisha nayo imechangia kuongezeka kwa ugonjwa huo, vijana wengi kwa sasa hutumia muda mwingi kuangalia video za ngono na staili zinazofanywa na wenzetu wa nje na hivyo kuongezeka kwa matumizi ya ngono ya mdomo.
Dk Kahesa anasema asilimia 12 ya wagonjwa wote wa saratani nchini wanasumbuliwa na saratani ya koo, hivyo kuna kila sababu kwa vijana kubadilisha tabia na kuepuka kuiga mitindo ya wenzetu wazungu ambayo mara nyingi inapotosha mila na tamaduni za Kiafrika.
Anasema katika mtiririko wa saratani zinazoongoza nchini saratani ya koo inashika nafasi ya tano, wagonjwa wengi wanaopatwa na ugonjwa huo ni watu wenye umri mkubwa wa miaka 60 na kuendelea hiyo inaonyesha kuwa wengi wao walianza ngono ya mdomo muda mrefu wakati wakiwa bado wadogo.
“Asilimia kubwa ya wagonjwa wanaopatikana na kansa ya koo nchini, inawapata watu wenye umri wa kuanzia miaka 60 na kuendelea kutokana na wengi wao kuanza mapema vitendo vya ngono kwa njia ya mdomo wakati bado wadogo au wengine kurithi kutoka kwa wazazi wao,” anasema Dk Kahesa.
Aina ya kansa ya koo
Tafiti zinaonyesha kuna aina mbili za saratani ya koo; aina ya kwanza ni “Oesophagus Carcinoma na Squamous cell carcinoma, zote hutofautiana wakati zinapimwa kwenye darubini lakini matibabu yake yanafanana.
Aina hizo ndizo zilizopo nchini na huanza mapema kuharibu seli ambazo zipo katika utandu uliopo katika ukuta wa koo kabla ya kuenea katika maeneo mengine ya koo.
Visababishi vya kansa ya koo:
Moja kati ya vitu vinavyosababisha kansa ya koo ni mwenendo wa maisha yetu kwa kula vyakula vyenye asidi, vyakula vichachu, vyakula vyenye pilipili, pombe kali na vyakula vigumu ambavyo hukwaruza koo na hivyo kusababisha saratani.
Anasema asilimia 90 ya wagonjwa wanaopokelewa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean road wanakuwa na historia ya kutumia vikali kama pombe kali, kuvuta sigara kwa kupindukia, kula pilipili kwa wingi na kutumia vitu vyenye uchachu.
Dalili za saratani ya koo
Moja kati ya dalili za mgonjwa wa saratani ni chakula kukwama kwenye koo, siku za mwanzo mgonjwa anaweza kushindwa kumeza chakula kigumu kisha cha majimaji na baadaye akashindwa kumeza hata mate.
Ugonjwa huo unachukua muda mrefu kugundua na kuona viashiria kwani mwanzo mgonjwa huanza kupata shida kumeza chakula na kwamba wagonjwa wengi wanaofika katika Taasisi hiyo ya Saratani wanakuwa tayari wamechelewa kwani wanakuwa katika hatua ya mwisho.
“Unaweza usionyeshe dalili lakini kadri siku zinavyokwenda ndiyo kunakuwa na dalili zinajitokeza pia katika kipindi hicho mtu anakuwa na maumivu wakati wa kumeza chakula, maumivu katika kifua na mgongo na hata kupungua uzito pamoja na kikohozi kikavu kinachoweza kudumu mwezi mmoja,” anasema.
Njia ya kuzuia saratani ya koo.
Kwanza mtu mwenye ugonjwa huo anapaswa kuhawi hospitali ili aanze matibabu mapema kutokana na ukweli kwamba mgonjwa anayewahi kupata matibabu ana uwezekano wa kupona kuliko yule ambaye amechelewa kugundulika na kuanza matibabu.
Kama saratani hiyo itakuwa imeshambulia viungo vyote vilivyopo jirani na koo na hadi kufika katika tezi au kiungo kingine cha mwili, mgonjwa anaweza kutibiwa kwa njia ya upasuaji, kutumia mionzi na hata kifaa maalumu ambacho ni kemikal

MC.RAY
WHATSAPP 0659/375263
INSTAGRAM MC.RAYMONDMUSHI
FACE BOOK Raymond Mushi
PAGE Rayshughuli



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni