Rais Jacob Zuma
Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini
amempongeza msichana Rolene Strauss wa A-Kusini alieshinda mashindano ya
urembo duniani yaliofanyika jana mjini London huku Chuo kiku anakosemea
msichana huyo A-Kusini kikimuandalia hafla kubwa ya kumpongeza
atakaporejea nyumbani .
Rolene Strauss aliibuka mrembo wa dunia wa mashindano ya Miss World 2014, akiwashinda zaidi ya warembo 120 kutoka kote duniani.Mshindi huyo wa shindano la Miss World 2014 alivikwa taji la urembo na mshindi wa Miss World 2013, Megan Young kutoka Ufilipino na kushangiliwa na mshindi wa pili na wa tatu, ambao ni Miss Hungary Edina Kulcsár na Miss Marekani Elizabeth Safrit.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni