1. Kukosa uaminifu katika mahusiano ya uchumba.
mojawapo ya matatizo yanayosababisha chumba nyingi kuvunjika
ni suala la kukosa uaminifu na hii hufungulia mlango wa shetani kuwashambulia
na hatimaye uchumba kuvunjika na wakati mwingine utawakuta wachumba wakiwa na
mahusiano ya kimapenzi na watu wengine na hii husababisha uchumba kuvunjika
hali ya kutamani maisha makubwa ambayo nje na uwezo
husababisha uchumba kuvunjika na wakati mwingine akijitokeza mtu mwingine
ambaye anaonyesha dalili fulani za kuwa na mali au pesa zaidi ya yule mchumba
huchangia kuvunjika kwa uchumba hivyo ni vizuri kulidhika na mchumba wako na
muanze pamoja na MUNGU atawabarikia mkiwa pamoja.
3.Kujihusisha na tendo la ndoa kabla ya ndoa.
Hili nadhani ni tatizo kubwa labda huenda kuliko haya
mengine na hili ni sumu kubwa sana inayovunja uchumba wa watu wengi, kwanza
huondoa imani kwa wale wachumba wenyewe, mtu anawaza huyu kakubali kufanya
mapenzi na mimi ipo siku atanichoka na kufanya na mwingine pia kufanya tendo la
ndoa kabla ya ndoa huweza kugundua baadhi ya madhaifu na mapungufu aliyonayo
mmoja wa wachumba hao na kuamua ikiwa hiki ndicho nakitarajia wakati ndoa mbona
nitakuwa nimejitwika tanzi? na hivyo huvunja uchumba na wakati mwingine
kuwatangazia watu madhaifu ya mchumba wake.
4.Kuanza kusemasema na kutangaza mapema kabla ya wakati
muafaka.
kutangaza juu ya uchumba wenu kabla ya hatua za awali
kumesababisha baadhi ya chumba kuvunjika unakuta hatua za awali kabisa kanisa
zima wanajua,kila mtaa wanajua yaani kila mtu anajua hii husababisha mmoja ya
wachumba kuona kuwa huyu mwenzangu hana siri na hawezi kutunza mambo huenda
hata tutakapooana hataweza kutunza siri hivyo anaweza kuvunja uchumba na wakati
mwingine kusemasema kabla ya muda huwasababisha wale walio maadui zenu
kuwazunguka kwa mbele na kupindua na ghafla unashangaa unakuta yule aliyekua
rafiki yako wa karibu uliye kuwa unamshirikisha jambo hilo kakuzunguka na
kukugeuzia kibao. Baada ya siku mbili tatu unaskia yuleyule mchumba wako
anamvisha pete mchumba wako.
5.Kuwasikiliza watu wengine zaidi ya kumsikiliza MUNGU.
Hii inaweza kusababisha uchumba kuvunjika. ni vizuri
kujifunza kumsikiliza MUNGU juu ya yule aliye kuongoza kwamba atafaa kuwa
mwenzi wako wa ndoa badala ya kuwasikiliza watu wanasema nini juu ya wewe na
mchumba wako. watu wanaweza kumtoa kasoro mfano mchumba mwenyewe hajasoma,ni
mbaya,hana figa nzuri,mchafu,hamuendani, maskini na kasoro nyingi tu na hiyo
husababisha uchumba kuvunjika
6.Kuchumbiana bila kumhusisha MUNGU.
Mlionana na kuvutiana pasipo kumhusisha MUNGU na kutangaza
kwa watu na kuanza mipango ya kuoana ndipo mnakuja kugundua kumbe ilikuwa ni
misisimko yenu tu wala MUNGU hakuhusika kabisa katika mchakato mzima wa uchumba
wenu na matokeo yake uchumba wenu unavunjika na kuacha ukijiuliza maswali
mengi.
7.kutumia muda mwingi katika uchumba kabla ya ndoa.
Kuna baadhi ya wachumba wanatumia muda mwingi sana kukaa
katika mahusiano ya uchumba kwa malengo ya kusomana tabia au kuchunguzana au
kusubiriana katika masomo nk. Hali hii hupelekea kuchokana katika mahusiano na
kuwasababishia kuona kama huenda labda nilichagua mtu asiye sahihi. Baada ya
kusoma na madhaifu mengi kwa muda mrefu mwisho uchumba huwezakuvunjika.


8.Roho ya haraka na kukosa uvumilivu.
Wengine wakichumbiana hupeleka mambo haraka haraka utadhani
ni dharula, wengi huwa na hali ya kutokujiamini huenda kutokana na yaliyowapata
siku za nyuma. labda walichumbiana na baada ya muda mfupi uchumba ukavunjika na
kuacha majeraha makubwa hivyo hudhani hali hiyo itajirudia, katika kufanya
mambo haraka huweza kusababisha hata huu uchumba kuvunjika.
9.Upinzani wa shetani ili ukose kilicho bora zaidi.
Kuvunjika kwa uchumba wakati mwingine kunaweza kusababishwa
na ibilisi shetani ambaye ni mdau wa kwanza wa upinzani juu ya mafanikio ya
wana wa MUNGU. Ndiyo maana tunahitaji sana kufunga na kuomba ili kuvunja na
kuharibu kazi za shetani na mipango aanayotuwazia sisi katika maisha yetu.
10.Uchumba kuvunjika kwa sababu ya mapenzi ya MUNGU.
Sio kila kitu kinaweza kusababishwa na shetani, wakati
mwingine MUNGU mwenyewe huingilia kati na kusababisha uchumba fulani kuvunjika
kutokana na sababu za kimungu ambazo wakati mwingine kwetu sisi sio rahisi
kuweza kuzijua kwa haraka mpaka wakati kamili wa MUNGU utimie au kusudi lake
kujidhihirisha wazi. Ni vizuri kwetu sisi kama watu wa MUNGU kutafuta mapenzi
ya MUNGU na kujua kwamba kuna wakati MUNGU mwanyewe anaweza kusababisha uchumba
kuvunjika kwa ajili ya usalama wetu.
- kumbuka NDOA SAHIHI NI YA MKE MMOJA NA MME MMOJA {MWANZO
2:24}
- pia NI DHAMBI KWA WACHUMBA KUFANYA TENDO LA NDOA KABLA YA
NDOA
- shetani ALIWADANGANYA ADAMU NA EVA KWA SABABU HAPENDI
MAFANIKIO KWA WANA WA MUNGU na hata huwadanganya wachumba wengi ili watende dhambi
kabla ya ndoa ili maisha yao ya ndoa yasiwe na baraka na pia ndoa hiyo
haitakuwa na ulinzi wa MUNGU jambo ambalo ni hatari.
-MUNGU akubariki sana ndugu na kumbuka kama hujampatia YESU KRISTO maisha yako unatakiwa ufanye hivyo leo maana pasipo yeye hakuna uzima wa milele (Yohana 14:6) na ukimshirikisha yeye hata kwenye uchumba wako yeye ni ngome imara na atakushindia yote.
-MUNGU akubariki sana ndugu na kumbuka kama hujampatia YESU KRISTO maisha yako unatakiwa ufanye hivyo leo maana pasipo yeye hakuna uzima wa milele (Yohana 14:6) na ukimshirikisha yeye hata kwenye uchumba wako yeye ni ngome imara na atakushindia yote.
-MUNGU akubariki sana
MC.RAY
WHATSAPP 0659/375263
INSTAGRAM MC.RAYMONDMUSHI
FACE BOOK Raymond Mushi
PAGE Rayshughuli
WHATSAPP 0659/375263
INSTAGRAM MC.RAYMONDMUSHI
FACE BOOK Raymond Mushi
PAGE Rayshughuli


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni