Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Jumanne, 9 Desemba 2014

UONGOZI WA rayshughuli.blogspot.com.UNAPENDA KUWATAKIA WATANZANIA WOTE KHERI YA MAADHIMISHO YA MIAKA 53 YA UHURU WA TANZANIA.


UHURU WETU NDIO DIRA YETU YA MAENDELEO
 Uhuru bila maendeleo hakuna uhuru haya ni maneno ya HAYATI BABA WA TAIFA KARIBU, Hivi vitu vinavyohusiana sana; uhusiano wao ni sawa na uhusiano baina ya kuku na yai!
OFISI YA KWANZA YA RAIS WA TANZANIA.MWL JK.NYERERE
 Bila ya kuku hupati mayai; na bila mayai kuku watakwisha. Vile vile, bila ya uhuru hupati maendeleo, na bila ya maendeleo ni dhahiri kwamba uhuru wako utapotea. Uhuru unategemea maendeleo. Tunapozungumza habari za uhuru maana yetu nini hasa, Kwanza, kuna uhuru wa nchi; yaani uwezo wa wananchi wa Tanzania kujipangia maisha yao, wakijitawala wenyewe bila ya kuingiliwa kati na mtu ye yote asiyekuwa Mtanzania. Pili, kuna uhuru wa kutosumbuliwa na njaa, maradhi, na umasikini. Na tatu, kuna uhuru wa mtu binafsi; yaani haki yake ya kuishi, akiheshimika sawa na wengine wote, uhuru wake wa kusema na uhuru wake wa kushiriki katika uamuzi wa mambo yote yanayogusa maisha yake, na uhuru wa kutokamatwa ovyo na kutiwa ndani kwa kuwa tu kamuudhi mkubwa, japo kama haku-vunja sheria yo yote. Yote hayo ni mambo yanayohusu uhuru, na hatuwezi kusema kuwa Wananchi wa Tanzania ni huru, mpaka tuwe tuna hakika kwamba wanao uhuru wa mambo yote hayo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni