
Unaporuhusu kitu chochote kisichotakiwa kuingia ndani ya uke wako,
unatoa nafasi ya kuharibu mfumo wake wa asili, na unajua ukishadisturb
mfumo wowote, athari zake ni chain reaction.
•Vidole vyako vinaweza kuwa na vijidudu (kumbuka uke ni msafi kuliko
vidole vyako) vijidudu hivyo vikashamiri na kuwashinda nguvu
Lactobacilli. Ukapata vaginal infections za kila namna.
•Kitendo hiki chaweza kupeleka vijidudu kwenye njia ya mkojo
ukasababisha UTI – Urinary Tract Infection
•Unawaua/kuwaondoa Lactobacilli na kuacha uke wako wazi na hatarini
kwa mashambuizi ya kila aina. Hakuna walinzi!!
•Mfumo wa uke usipofanya kazi vizuri ndio utaona ute mwingi kuliko
inavyotarajiwa au mkavuuuu kabisa.
•Uchafu wowote mwingine unashindwa kusafishwa naturally unalundikana
matokeo yake ofcousre infections na harufu mbaya.
•Amini usiamini ni sababu mojawapo inayoleteleza saratani ya shingo ya uzazi.
•Mashambulizi mengine yanasaabisha utasa (infertility)
•Ute unakauka, na pale unapouhitaji (tenda la ndoa) hautakuwepo na
kusababisha michubuko ambayo inaongeza fursa za maambukizi ya magonjwa
ya ngono.
He? Sasa tusafishe vipi uke kuhakikisha una afya njema?
•Safisha nje tu kila siku unapooga au unapojisikia kwa maji safi na
mikono misafi. Nje ya uke kunahusisha mashavu na katikati yake.
•Waweza kutumia sabuni isiyokua na kemikali kali, japo haishauriwi pia
HII NI SEHEMU TU YA SOMO LITAENDELEA LAO USIKU USIKOSE.......
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni