Putin akitoa hotuba yake kwa taifa kupitia televisheni
Rais Vladmir Putni wa Urusi ametumia
hotuba yake ya kila mwaka kwa taifa kushambulia mataifa ya Magharibi
ambayo amesema yamekuwa na unafiki mkubwa juu ya hali ilivyo nchini
Ukraine.
Bwana Putin alisema kuwa kama pasingekuwa na matatizo
Ukraine wakati huu mataifa ya Magharibi bado yangalikuja na swala
lingine la kujaribu kudhibiti Urusi.Alisema pia kuwa Urusi haitakubali kusambaratika jinsi ilivyofanyika katika taifa la Yugoslavia.
Bwana Putni alisema kuwa Uchurmi wa Urusi unakabiliwa na changamoto nyingi siku za mbeleni, lakini akasisitiza kuwa vikwazo hivyo vitasaidia Urusi kuunda mbinu mwafaka za kujitegemea.
Rais aliwahimiza waekezaji kurudi tena Urusi kwa kutangaza kuwa hakutakuwepo na upekuzi juu ya uhalifu wa fedha au kama kulikuwepo na wizi wa kodi juu ya rasilmali itakayoingizwa nchini.
Alisema Urusi ni mahali salama zaidi kwa Warusi kuhifadhi pesa zao
CHANZO BBC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni