Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Jumatatu, 15 Desemba 2014

WAANDAMANAJI WAPAMBANA NA POLISI MEXICO.


Ndugu na jamaa wana imani ya kuwapata wapendwa wao
Polisi nchini Mexico wamepambana na Waandamanaji walioandaa tamasha mjini Chilpancingo wakikumbuka kundi la Wanafunzi 43 waliopotea zaidi ya miezi miwili iliyopita.
Polisi wamesema maafisa kadhaa wamejeruhiwa, wakiwemo baadhi waliogongwa na gari.
Makundi hayo mawili yameshutumiana kuanza machafuko siku ya jumapili.
Tukio la kupotea kwa Wanafunzi, mmoja kati yao kuokotwa akiwa amepoteza maisha, kulizua maandano sehemu zote nchini Mexico.
Vurugu zilijitokeza baada ya Waandamanaji kuweka vizuizi katika mtaa mjini Chilpancingo kabla ya tamasha lililopangwa kufanyika.
Tamasha liliahirishwa baada ya vurumai hizo,wakati huo,magari kadhaa yalichomwa moto.
Kundi la Wanafunzi 43 kutoka taasisi ya mafunzo ya ualimu mjini Ayotzinapa lilitoweka tarehe 26 mwezi Novemba baada ya kupambana na Polisi wa manispaa ,mjini Iguala.
Inadaiwa kuwa wanafunzi 43 walichomwa moto katika jalala la takataka baada ya kubaini kuwa wanafunzi hao walikuwa kwenye kundi hasimu.
Uchunguzi uliofanywa kwa mfupa uliookotwa kwenye mto karibu na jalala umeonyesha kuwa ni Kiungo cha mmoja wa Wanafunzi 43 waliopotea.
Ndugu wa Wanafunzi hao wamesema hawatakata tamaa wakiwa na matumaini kuwapata.
CHANZO BBC.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni