Wanawake makahaba wa India
Polisi Mashariki mwa mji wa Calcutta
nchini India, wanachunguza tukio la mwanamke ambaye jamii yake
ilimtelekeza katika bwawa,kwa kushindwa kuzaa mtoto wa kike ambaye
baadaye walimtegemea kuwa kahaba.
Mwanamke huyo aliokolewa na chama cha kujitolea kuwahudumia makahaba kabla hajalazimika kujitosa kwenye ukahaba kamili.Mwanamke huyo aliiambia BBC kwamba familia ya wakwe zake walianza kumdhihaki baada ya kuzaa watoto wa kiume watatu mfululizo, na kufahamishwa kwamba familia hiyo kwa kawaida huwapeleka watoto wa kike wa ukoo wao kufanya kazi ya ukahaba, iweje yeye azae watoto wakiume watupu?.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni