Polisi nchini Brazil wamefanya
uvamizi kwenye majimbo sita katika oparesheni kubwa ya kuchunguza
ufisadi kwenye kampuni ya mafuta ya serikali ya Petrobras.
Watu 18
walikamatwa wakiwemo wakurugenzi wakuu wa makampuni makubwa ya ujenzi
nchini brazil wanaoshutumiwa kwa kutoa hongo ili kujishindia kandarasi
za pesa nyingi za kampuni hiyo ya mafuta.Mkurugenzi wa zamani wa Perobras Renato Duque pia alikamatwa kwenye oparesheni hiyo iliyowajumuisha zaidi ya polisi 300.
Uchunguzi huo ulianza mapema mwaka huu wakati mkurugenzi mkuu wa zamani wa kampuni hiyo ya mafuta aliposema kuwa moja ya idara za kampuni ililipa mamilioni ya dola kwa wanasiasa wakiwemo wanachama wa chama tawala cha workers party
chanzo BBC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni