Tottenham wanafanya mipango ya
kuwapata kiungo Morgan Schneiderlin,25 pamoja na mshambuliaji Jay
Rodriguez, 25,wote toka klabu ya Southampton na beki wa Raul Albiol,
29,wa Napol ya Itali ili kuimarisha kikosi chao.
Leicester City
wamekata ofa ya £7.9milioni kuweza kumuuza mshambuliaji wao Andrej
Kramaric, the 23 raia wa Croatia anawaniwa na timu za Chelsea na
Tottenham.Kocha wa Sunderland Gus Poyet bado anamuhitaji mshambuliaji Fabio Borini, 23, aliekosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Liverpool.
Bosi wa Newcastle Alan Pardew anataka kumsajili kwa mkopo kipa Mark Schwarzer, kutoka chelsea ambae ni chaguo la tatu kwa kocha Jose mourinho.
Harry Redknapp kocha wa QPR ana imani atamsajili kwa mkopo mshambuliaji Robbie Keane, 34, nyota wa zamani wa Tottenham anayechezea timu ya LA Galaxy ya Marekani.
CHANZO BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni