Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Jumatatu, 8 Desemba 2014

MAELFU WAHITAJI MSAADA SOMALIA



Hali mbaya ya usalama nchini Somalia inachochea hali mbaya ya kibinadamu
Umoja wa Mataifa unasema kua zaidi ya watu milioni tatu wanahitaji msaada wa dhahura kwa sababu ya tatizo kubwa la utapia mlo na mgogoro.
Tahadhari hio imetolewa miaka mitatu baada ya zaidi ya robo ya watu milioni moja kufariki kutokana na ukosefu wa chakula.
Katika taarifa yake ofisi ya mratibu wa misaada ya kibinadamu katika Umoja wa Mataifa inasma kuwa wasomali wanaendelea kukabiliwa na hali ngumu ya kibindamau.
 
Ukame na uhaba wa chakula limekuwa tatizo kwa wengi Somalia inayokumbwa na vita
Maelfu ya watu wameathirika kutokana na vita vinavyosababishwa na wanamgambo wa Al Shabaab.
Kikosi cha wanjeshi wa Muungano wa Afrika kiko nchini humo kuoambana na wanamgambo hao.
Wadadisi wanasema hali hiyo imechocewa zaidi na ukame pamoja na mafuriko katika baadhi ya sehemu za nchi hio.
CHANZO BBC

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni