Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Jumatatu, 8 Desemba 2014

KABILA AINGIZA WAPINZANI SERIKALINI.



Wadadisi wanasema Kabila analenga kuangamiza upinzani
Rais wa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, Joseph Kabila amebuni serikali ya Muungano ambayo inajumuisha viongozi kadhaa wa upinzani.
Afisaa mkuu wa chama cha upinzani cha '' Movement for the Liberation of Congo'' ametajwa kama naibu waziri mkuu.
Viongozi wengine wa zamani wa upinzani pia wamepewa nyadhifa katika serikali hio.
Serikali hio ya Muungano, imebuniwa huku kukiwa na wasiwasi kuwa Bwana Kabila, ambaye amekuwa mamlakani tangu mwaka 2001, anaweza kujaribu kubadilisha katiba ili awanie muhula wa tatu.
Wadadisi wanasema kuwa kujumuishwa kwa wapinzani katika serikali ya muungano inawezekana ni njama ya kuongeza ufuasi wake na kudidimiza upinzani.
Wanaongeza kuwa hatua ya Kabila ni ya kujiandaa kwa mageuzi ya kikatiba au hata kuchelewesha uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka 2016.
Evariste Boshab, kiongozi wa chama cha (People's Party for Reconstruction and Democracy), pia ametajwa kama naibu waziri mkuu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni