6. Mwanaume mwenye
utititri wa watoto kila kona:
Mwanaume kuwa na watoto nje ya ndoa si jambo la
kushangaza siku hizi, lakini pale unapokutana na mvulana mwenye umri wa miaka
25 lakini ana watoto watatu kwa mama tofauti, mh! hapo sikushauri ujiingize
kwenye uhusiano na mwanaume huyo. Hata hivyo si lazima awe na miaka 25 tu hata
mwanaume mwenye umri mkubwa zaidi ya huo halafu ana watoto watatu au hata wanne
au zaidi kutoka kwa mama tofauti ni wa kuepuka. Hivi atakupa sababu gani
zilizomfanya akawa na watoto kwa mama tofauti kila kona ya mtaa mpaka umuelewe!
Kuwa na mahusiano na mwanaume aina hiyo ni kukaribisha shari nyumbani kwako
maana kila siku utapata wageni wanaokuja kudai hela za matumizi kutoka kwa
mumeo tena wengine watakuja kishari hasa na kukuharibia siku. Mh mh! sikushauri
mwanamke, sepa zako, bado nafasi unayo ya kumpata mwanaume mwingine mwadilifu.,,,,,,LINAENDELEA MUDA SI MREFU HIKI NI SEHEMU TU.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni