Malala Yousafzai
Mshindi wa Nishani ya Nobel bint Malala Yousafzai raia wa Pakistani amesema kuwa siku zijazo anatarajia kuwa mwanasiasa.
Malala
amesema ndoto yake hiyo anatarajia kuikamilisha baada ya kumaliza
masomo yake na amesema ikiwezekana anapenda kuwa Waziri Mkuu wa nchi
hiyo.Binti huyo ambaye amekuwa akiendesha kampeni ya elimu dhidi ya wasichana alipigwa risasi na wapiganaji wa Talban miaka miwili iliyopita.
Mshindi huyo wa Nobel Malala yupo mjini Oslo ,Norway anatarajiwa kupokea Nishani anayoshirikiana na Bindi raia wa India Kailash Satyarthi
CHANZO BBC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni