Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Jumatano, 10 Desemba 2014

SOMO LA LEO.SIMU YAWEZA KUVUNJA NDOA/ UHUSIANO WAKO







Leo napenda tujadiliane suala la simu za mkononi. Suala hili bilashaka limeshazungumzwa mara nyingi sana katika vyombo mbali mbali vya habari, simu za mkononizina faida nyigi tu ila wahenga walisema “kila lenye faida halikosi hasara”, lakini mimi napenda kuingia ndani zaidi na kulihusisha na suala la mahusiana kati ya wapendanao.
Unawezaje kuyafanya  mahusiano yako yadumu na yasivunjike kwa sababu tuu ya simu yako au ya mwenza wako?
Watu wengi sana wamekuwa wakijikuta katika wakati mgumu kwa sababu ya kitu hiki kidogo, simu!!! Hebu jiulize! “kwanini wewe unamiliki simu yako na ya mpenzi wako? kwanini humuamini? kwanini nawe pia hujiamini?  Je kama anakupenda kwa dhati anaweza kukudanganya? kwa nini usimpe nafasi ajitambue kuliko kuwa mlinzi wa simu yake? Unahisi wewe ukijua anawasiliana na nani kutwa nzima ndo utakuwa na furaha maishani au utaongeza matatizo moyoni mwako na katika mahusiano yenu?
Maswali hayo machache tujiulize kabla hatujaenda mbali. WHY? KWANINI?
Katika hali ya kawaida tu ukikagua simu ya mweza wako kila wakati utajikuta badala ya kupata faraja moyoni unajikuta unapata stress ambazo hazina mpango!! Unaumiza moyo wako maana utajikuta unagundua vitu vingi vya ajabu na mahusiano yanaanza kuvurugika!
.
 JE! NI NINI SULUHISHO?



Uaminifu ni kitu kizuri, muonyeshe kuwa unamuamini sana. usimfuatilie kupita kiasi hasa katika simu yake ya mkononi. Mwache awe na uhuru na simu yake, muonyeshe kuwa bila yeye unaweza kuishi maana ukifuatilia sana simu yake, utaumia na atabaini kuwa bila yeye hujiwezi sikio wala ndewe!!
Unajua mtu ukimpa uhuru sana hata yeye anajishtukia na kushangaa inakuwaje, kwa hiyo hata kama anafanya ujinga atajirudi kwa kuona ni kiasi gani anakukosea na wakati wewe umetulia na unampenda.
Mpende kwa dhati, lakini haimaanishi ndo uwe mlinzi wa simu yake ya mkononi, utajiumiza 


MC.RAY
WHATSAPP 0659/375263
INSTAGRAM MC.RAYMONDMUSHI
FACE BOOK Raymond Mushi
PAGE Rayshughuli

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni