Wanamgambo wa Islamic State, wanaolengwa kushambuliwa.
Muungano wa majeshi yanayopambana dhidi ya Islamic State yakiongozwa na Marekani, yako tayari kupeleka vikosi zaidi nchini Iraq.
Kamanda
wa muungano wa majeshi hayo, Jenerali James Terry kutoka Marekani
amesema kiasi cha wanajeshi elfu moja na mia tano wataanza kupelekwa kwa
ajili ya kutoa mafunzo kwa wanajeshi ya Iraq, wanaopambana na
wanamgambo wa kiislamu.Idadi ya washauri hao wa kijeshi itaongezwa kati ya wanajeshi wa Marekani zaidi ya elfu tatu, ambao Rais Obama tayari amewaidhinisha kupelekwa Iraq.
Bado haijawekwa wazi wanajeshi wengine wa ziada watatoka katika mataifa yapi.
CHANZO BBC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni