maandamano drc
Mkuu wa kanisa katoliki nchini Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo ameunga mkono maandamano ya kupinga mabadiliko katika ya sheria ya uchaguzi ambayo imezua siku tatu za maandamano.
Kadinali laurent Monsengwo ameitaka mamlaka kwa maneno yake mwenyewe kusitisha mauaji ya raia wake.
Amewataka waandamanaji kuweka amani.
Makundi ya haki za kibinaadamu yamesema kuwa zaidi ya watu 40 wamefariki katika ghasia hizo.
Vyama vya upinzani vinasema kuwa sheria hiyo iliyopendekezwa ililenga kuchelewesha uchaguzi ili rais Joseph Kabila aendelee kuwa mamlakani baada ya kipindi chake cha utawala kuisha mwaka ujao.
CHANZO BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni