Mchezaji wa Real Madrid Ronaldo asema hatojiunga na Chelsea wala Man United
Mchezaji bora duniani kutoka kilabu
ya Real Madrid Christiano Ronaldo amewavunja moyo mashabiki wa kilabu ya
Manchester United na Chelsea baada ya kusema kuwa anapania kwenda
Brazil kusakata kabumbu baada ya kutoka Real Madrid kulingana na gazeti
la Metro.
Mchezaji huyo ambaye anatabiriwa na wengi kurudi katika
kilabu ya Manchester United baada ya kumaliza mkataba wake na Real
Madrid amesema huenda akaichezea kilabu ya Corinthians ama hata Flamengo
nchini Brazil atakapoondoka Real Madrid.''Corinthians na Flamengo ni vilabu maarufu ambavyo huenda nikachezea moja wapo.nchini Brazil nina marafiki wengi kwa hivyo uhusiano wangu na taifa hilo ni mzuri sana.''alisema Ronaldo.
CHANZO BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni