Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Jumamosi, 17 Januari 2015

USA KUAMUA KUHUSU NDOA ZA JINSIA MOJA


Mahakama ya Marekani kufanya uamuzi wa jumla kuhusu ndoa za jinsia moja nchini humo
Mahakama kuu nchini Marekani inatarajiwa kutoa uamuzi wa nchi nzima iwapo wapenzi wa jinsia moja wana haki ya kufunga ndoa.
Mahakama hiyo itatathmini suala hilo kwenye majimbo ya Kentucky, Ohio, Michigan, na Tennessee kati ya majimbo mengine 14 ambayo yamepiga marufuku ndoa za jinsia moja.
Mahakama hiyo pia itaamua ikiwa majimbo yatatambua ndoa za jinsia moja kutoka sehemu nyengine nchini humo.
Kukubaliwa kwa ndoa za jinsia moja kumeshuhudiwa nchini Marekani miaka ya hivi karibuni suala ambalo linaungwa mkono pakubwa na chama cha Democratic huku likikigawanya chama cha Republican.
CHANZO BBC

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni