Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Jumapili, 25 Januari 2015

18,WAUAWA MISRI.


Waandamanaji Misri
Serikali ya Misri imesema watu kumi na wanane akiwemo Polisi mmoja wameuawa wakati wa maandamano yaliyofanyika nchini humo wakati wakiadhimisha miaka minne tangu kuangushwa utawala wa Hosni Mubarak.
Vifo hivyo vimetokea mjini Alexandria na cairo,Serikali ilipiga marufuku kuadhimisha kumbukumbu hizo hali iliyosabbaisha vurugu kati ya Waandamanaji na Polisi.
Zaidi ya watu 400 pia wanashikiliwa kutokana vurugu hizo.Hata hivyo serikali ilipiga marufuku tukio hilo linalodaiwa kuwa ni la kumbukumbu ya maandamano 2011.
Maandamano hayo ya mwaka 2011 nchini Misri yalikuwa yakiratibiwa na makundi ya Waislam wenye msimamo mkali ambapo vikosi vya usalama vilishindwa kuwadhibiti waandamanaji hao
CHANZO BBC

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni