Mazao ya samaki
Mabadiliko ya hali ya hewa yamekuwa
yakileta madhara duniani ,nchini Tanzanian mamlaka ya hali ya hewa
imelazimika kutoa taarifa maalumu kwa umma kuhusiana na tahadhali ya
mabadiliko ya hali hewa katika ukanda wa Pwani kutokana na kuimarika kwa
mgandamizo mdogo wa hewa katika eneo la Bahari ya hindi mashariki mwa
kisiwa cha Madagascar hali inayoleta mawimbi makali.
Shughuli ya
uvuvi katika bahari ya Hindi ni tegemeo kwa uchumi na huduma ya
samaki,lakini kwa sasa mambo yamebadilika samaki wanapatikana kwa tabu
kufuatia wavuvi kuogopa kuingia Baharini kuvua,huku hali ya usafiri kwa
vyombo vya majini ndani ya Bahari hiyo vikikumbwa na hali mbaya kutokana
na mawimbi makali.Hali hiyo ya kuchafuka kwa bahari na hali ya hewa, pamoja na mawimbi makali bahari ya Hindi, ni kilio kikubwa kwa wavuvi wa mwambao huo wanaoendesha maisha yao kwa kutegemea uvuvi, kwani kwa sasa samaki hawapatikani tena kama hapo awali.
Kutokana na mabadiliko hayo ya hali ya hewa,imeathiri upatikanaji wa mazao ya samaki na sasa bidhaa ya samaki imepanda bei kutoka elfu kumi ama ishirini kwa ndoo ya lita kumi hapo awali sasa inauzwa kwa elfu sabini kwa dagaa mchele, na hivyo kumfanya mjasiriamali mwenye kipato cha chini kutomudu kununua bidhaa hiyo.
CHANZO BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni