Marekani imelaani hatua ya mahakama
ya kimaitaifa ya uhalifu wa kivita ICC kuanzisha uchunguzi kuhusu
uwezekano wa kuwepo kwa uhalifu wa kivita kwenye utawala wa Palestina.
Msemaji
wa wizara ya ndani nchini Marekani anasema kuwa ni jambo lisiloaminika
kuwa Israeli ambayo imekuwa ikishambuliwa kwa makombora yanayofyatuliwa
katika ardhi yake kuwa sasa ndiyo inayochunguzwa na ICC.Mapema Isreal iliitaja hatua hiyo kama yenye lengo la kuizuia isijilinde kutokana na vitendo vya kigaidi.
Uchunguzi huo ambao ICC inasema utakuwa huru utatumiwa kuamua iwapo kutafanyika uchunguzi ulio kamili.
CHANZO BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni