Msako barani ulaya kuwatafuta watu wenye itikadi kali za kidini
Polisi katika nchi kadhaa barani
Ulaya wamewakamata washukiwa kadhaa wenye iktikadi kali za kidini katika
misako iliyofanywa usiku kucha.
Ripoti kutoka nchini Ufaransa
zinasema kuwa washukiwa wanane wametiwa mbaroni, kuhusiana na
mashambulio ya wiki iliyopita ambako watu kumi na saba waliuawa.Afisa mmoja wa serikali ya nchi hiyo amesema kuwa washukiwa hao wanaendelea kuhojiwa kuhusiana na madai ya kuwasaidia washambuliaji kwa kuwabebea silaha au kuwapa usafiri .
Nchini Ujerumani, polisi wamewakamata washukiwa kadhaa wa ugaidi baada ya kufanya opereshenu kali mjini Berlin.
Duru zinasema kwamba misako yote ilifanyika katika mtaa mmoja wa Kusini mwa Paris ambako mmoja wa washambuliaji alikulia.
Nchini Ujerumani, polisi wamewakamata washukiwa wa kundi la kigaidi baada ya kufanya misako mingine ndani na katika maeneo yanayozingira mji wa Berlin.
Hata hivyo polisi walisema hawakupata ushahidi kwamba walikuwa wanajiandaa kufanya mashambulizi nchini Ujerumani.
CHANZO BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni