Maandamano Niger
Watu watano wameuawa kwenye mji mkuu
wa Niger, Niamey ikiwa ni siku ya tatu ya maadamano ya kupinga
kuchapishwa kwa kibonzo cha mtume Mohammed na gazeti la kila wiki nchini
Ufaransa la Charlie Hebdo.
Karibu vijana 1000 waliokuwa wamebeba
chuma na shoka waliandamana kwenye barabara za mji huo wakiwarushia
polisi mawe ambapo walijibu kwa kurusha vitoa machozi.Waandamanaji hao walichoma moto karibu makanisa 7 mjini Niamey.
Maiti mbili zilizokuwa zimekatwakatwa zilipatikana ndani ya kanisa moja lililokuwa limeteketezwa moto.
Picha za runinga zilionyesha waandamanaji wakirarua biblia wakisema Allahu Akbar huku wakipeperusha Koran.
Baadhi ya biashara za Ufaransa nazo zilivamiwa yakiwemo maduka ya kampuni ya simu ya Orange.
Ubalozi wa Ufaransa nchini humo umewashauri raia wake walio mjini Niamey kusalia majumbani mwao.
CHANZO BBC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni