Rais Salva Kiir
Mkutano wa viongozi wa kikanda
ulioandaliwa kujadili mgogoro wa mwaka mmoja unaotokota nchini Sudan
Kusini, umecheleweshwa baada ya Rais Salva Kiir kuugua na kukimbizwa
hospitalini mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Afisa mmoja wa shirika la
IGAD, ambalo linafanya juhudi za kuwakutanisha viongozi wa Sudan Kusini
kwa lengo la kumaliza vita, aliambia BBC kwamba Rais Kiir, alianza
kuvuja damu kutoka puaniKabla ya kuugua, hapo jana Kiir alifanya mazungumzo na kiongozi wa waasi Riek Machar ambapo alimtaka kupuuzilia mbali maswala yanayochochea mgogoro huo ili kumaliza mgogoro huo ambao umedumu mwaka mmmoja
Viongozi wa kikanda, wanakutana baadaye leo, kushinikiza pande zote kufikia makubaliano ili kumaliza vita.
Swala kuu kwenye ajenda, ni kusuluhisha maswala yanayoleta kizungumkuti kuhusu serikali ya muungano kama moja ya suluhu la kupatikana amani.
Pande zote zinazozozana zimekosa kufikia makubaliano kuhusu wadhifa wa waziri mkuu na ikiwa anapaswa kuwa na mamlaka makuu au la.
Maelfu ya watu wamefariki na wengine zaidi ya milioni moja kuachwa bila makao tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe kuzuka nchini humo Disemba mwaka 2013.
CHANZO BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni