Libby Lane kuwa kasisi wa kwanza mwanamke
Kanisa moja nchini Uingereza hii leo limemuapisha mwanamke wa kwanza kuwa kasisi.
Mchungaji
Libby Lane kama anavyojulikana sasa atakuwa kasisi wa Stockport katika
sherehe iliofanyika katika eneo la York Minster,ikiwa ni miezi sita tu
baada ya kanisa hilo kumpigia kura ili kumaliza utamaduni wake wa
wanaume kuwa makasisi.Kasisi huyo amesema kuwa iwapo uchaguzi wake utawafanya wanawake kubaini uwezo wao basi anafurahia.
Hatua hiyo imeendelea kuzua hisia tofauti miongoni mwa wafuasi wa kanisa hilo la kianglikana duniani.
CHANZO BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni