Mkuu wa Shirika la Afya Duniani,
WHO, ameeleza mpango wa kuliimarisha shirika hilo baada ya malalamiko
mengi kuhusu namna WHO ilivyoshughulikia mripuko wa Ebola Afrika
Magharibi, ambayo imeuwa watu zaidi ya 8,000.
Margaret Chan alielezea mripuko huo kuwa maafa ambayo ni funzo kubwa kwa ulimwengu na WHO.
Katika kikao cha viongozi wa WHO mjini Geneva, Bibi Chan alisema mbinu za kupambana na misukosuko kama hiyo zinafaa kuimarishwa na kuanzishwe mfuko wa kugharimia hali ya dharura.
Alisema maafa ya Ebola yameonesha piya kwamba mfumo mwema wa afya wa taifa ni kitu cha lazima, siyo anasa.
CHANZO BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni