Maandamano nchini Pakistan kuonyesha kero la waumini wa kiisilamu kuhusu Charlie Hebdo
Polisi nchini Pakistan wamekabiliana
na waandamanaji, walioghadhabishwa na uamuzi wa jarida na Ufaransa la
Charlie Hebdo wa kuchapisha vibonzo vya mtu wanayedai ni Mtume Mohammad.
Baada
ya maombi ya ijumaa, maafisa wa ulinzi walitumia magari yenye majai
kuwamwagia maji waandamanaji katika juhudi za kuwatwanya.Walikuwa wamekusanyika nje ya ubalozi wa Ufaransa mjini Karachi.
Baadhi ya waandamanaji inaarifiwa walikuwa wamebeba bunduki. Watu watatu walijeruhiwa katika maandamano yenyewe.
Mwandishi wa BBC mjini Islamabad amesema idadi ya waandamanaji hao, kwa mujibu wa idadi ya wasisilamu nchini Pakistan, ilikuwa ndogo.
Maandamano kama hayo yameitishwa katika nchi zingine zilizo na idadi kubwa ya waumini wa Kiislamu kama vile Uturuki, Ufilipino,Kuwait, Mauritania na Sudan.
chanzo bbc
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni