Hoteli ilioshambuliwa
Kumekuwa na shambulizi la mlipuaji
wa kujitolea muhanga katika hoteli moja mjini Mogadishu nchini Somali
ambapo maafisa wa Uturuki walikuwa wakijiandaa kumlaki rais Recep Teyyip
Erdogan.
Takriban raia watatu wa Somali waliuawa wawili kati yao
wakiwa maafisa wa usalama wakati gari lililojaa vilipuzi lilipogonga
lango la hoteli.Uturuki hatahivyo imesema kuwa hakuna mjumbe wake aliyejeruhiwa na kwamba ziara ya rais Erdogan itaendelea kama ilivyopangwa siku ya ijumaa.
Kundi la wapiganaji wa Alshabaa limesema kuwa lilitekeleza shambulizi hilo.
CHANZO BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni