Senegal yaichapa Ghana
Mshambuliaji wa Senegal Moussa Sow
alifunga bao la mda wa lala salama na kuisaidia Senegal kupata ushindi
dhidi ya Black stars ya Ghana.
Mchezaji huyo aliyeingia dakika za
mwisho za mechi hiyo alifunga bao lake kunako dakika ya 90 na kuipatia
timu yake alama zote tatu.Mchezaji wa Ghana Andrew Ayew alifunga mkwaju wa Penalti baada ya kiungo wa kati wa Everton Christian Atsu kuangushwa katika eneo la hatari.
Lakini Senegal ilijitahidi na kupiga chuma cha goli la Ghana kupitia mchezaji Kara Mbodj,kabla ya mshambuliaji wa Stoke Mame Biram Diouf kufunga bao la kusawazisha huku Mousa Sow akifunga bao la Ushindi.
CHANZO BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni