Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Jumanne, 20 Januari 2015

VURUGU KUMPINGA RAIS KABILA DRC


Polisi katika Jamuhuri ya kidemokrasi ya Congo, wamefyatua risasi hewani ili kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wamekusanyika katika mji mkuu Kinshasa kupinga sheria mpya ya uchaguzi.

Serikali inasema kuwa watu wanne walifariki katika vurugu za Jumatatu ingawa upinzani unasema idadi huo huenda ikwa kujuu kuliko iliyonakiliwa.
Wanafunzi wameweka vizuizi barabarani na pia wameshuhjudiwa wakichoma magurudumu, katika barabara zinazoelekea katika chuo kikuu mjini humo.
Wanatuhumu wanasia wanaomuunga mkono Rais Joseph Kabila ambaye muhulka wake wa pili unatarajiwa kumalizika mwaka ujao kwa kujaribu kujiongeza muda mamlakani kwa kuidhinisha mipango ya kufanyika sensa ambayo itachelewesha uchaguzi kwa miaka mingi.
Vurugu hizi zinashuhudiwa huku baraza la Senate likidadisi mswada ambao huenda ukasababisha Rais Kabila kuongezwa muda mamlakani.
 Waandamanaji wanamtuhumu Rais kwa kufanya wanachokiita mapinduzi ya kikatiba
Vijana walioandamana kwa vurugugu, waliteketeza magurudumu ya magari, kupora maduka na kurusha mawe.
Wanafunzi waliambia BBC kuwa polisi walivamia chuo chao baada ya wao kuanza kuandamana.
Walisema polisi walingia katika vyumba vyao na kuwafyatulia gesi ya kutoa machozi.
Viongozi wa upinzani walitoa wito kwa waandamanaji kwenda barabarani kupinga mipango ya serikali kumuongeza muda zaidi mamlakani Rais Joseph Kabila huku wakiutaja mpango huo kuwa mapinduzi ya kikatiba.
Mswada huo unapendekeza kufanytika sensa kote nchini ambayo itachukua kipindi cha miaka mitatu.
Rais Kabila amekuwa mamlakani tangu mwaka 2001. Muhula wake wa pili unakamilika mwaka 2016 kikatiba.
CHANZO BBC

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni