Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Jumanne, 6 Januari 2015

DAR JIJI GHALI KUISHI


Wakazi wa Dar es Salaam hutumia gharama kubwa kufanya manunuzi
Wakazi wa jiji la Dar es Salaam hutumia gharama kubwa zaidi, kulipia mahitaji yao ya muhimu kuliko wenzao wengine wa Afrika mashariki, jijini Nairobi na Kampala,utafiti uliofanywa na Shirika linalotathimini gharama za maisha,Numbeo umeeleza.
Utafiti huu ulifanywa ukihusisha miji mikubwa 22 ukiangalia uwezo wa kununua bidhaa,biashara za migahawani, hali kadhalika utafiti huu ulijikita kwenye gharama za juu na urahisi wa maisha ya mijini
Kwa mujibu wa Ripoti ya Numbeo , takwimu za gharama za watumiaji kwa wakazi wa Dar es Salaam kwenye bidhaa na huduma mbalimbali ni asilimia 62.83 ambayo imezidi Kampala na Nairobi zenye asilimia 54.34.
Kwa sasa Kenya ni nchi inayoongoza kwa kuwa na uchumi mkubwa Afrika Mashariki na iko nafasi ya sita barani Afrika, hata hivyo kwa mujibu wa matazamio ya Benki ya Standard Charterd , Tanzania inaelekea kuipiku Kenya na kuwa nchi yenye uchumi mkubwa ifikapo mwaka 2030 iwapo pato la taifa halitabadilika.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni