Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Jumatatu, 5 Januari 2015

EBOLA;DRC YATUMA WATABIBU GUNEA


Wafanyakazi wa Afya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wakihudumia wagonjwa
Wafanyakazi wa afya 81 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wamewasili nchini Guinea, kusaidia kukabiliana na janga la Ebola.
Timu hiyo ni pamoja na madaktari, wauguzi, wataalam wa maabara, saikolojia na mawasiliano.
Wataalamu hao wataanza kazi moja kwa moja katika vitengo husika na kutibu ugonjwa wa Ebola nchini Guinea.
Pia watatoa mafunzo kwa wafanyakazi wa afya wa mitaa ya nchi hiyo kuhusu namna ya kuzuia kuenea kwa virusi vya Ebola nchini humo.
Wakati huo huo Shirika la Afya Duniani limetoa takwimu mpya za mlipuko wa Ebola. Kwa mujibu wa shirika hilo vifo vilivyotokana na Ebola katika nchi tatu zilizoathirika zaidi imepita watu 8,000.
Takwimu hizo mpya ni kwa nchi za Sierra Leone, Guinea na Liberia pekee. Watu 8,153 wameripotiwa kufa, ambapo watu 20, 656 wameugua ugonjwa huo katika nchi hizo tatu.
Takwimu zinaonyesha kuwa Sierra Leone - imekuwa na wagonjwa 9,772 na vifo 2,915. Liberia wagonjwa 8,115 na vifo 3471 ambapo Guinea imeripotiwa kuwa na wagonjwa 2,769 na vifo 1,767.
Takwimu hizo ni hadi kufikia Desemba 31 kwa upande wa Liberia, na kwa upande wa nchi za Sierra Leone na Guinea takwimu hizo ni hadi Januari 3, 2015.
Pia nchini Mali kuna taarifa za wagonjwa 8 na vifo vya watu 6. Ambapo Uingereza ina mgonjwa mmoja na hakuna kifo.
CHANZO BBC

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni