Mtu anayetumia mtandao wa facebook kwa mawasiliano
Mitandao ya Twitter na facebook
imekataa kuchapisha mamia ya jumbe za chuki licha ya kutakiwa kuchapisha
jumbe hizo na makundi ya ubaguzi .
Kulingana na uchunguzi
uliofanywa na gazeti la The Independent nchini Uingereza, idadi ya jumbe
baadhi yao zikiwa zinawashtumu waislamu kwa kuwa wabakaji na
kuwafananisha na ugonjwa wa saratani zimeongezeka kwa kiwango kikubwa
katika kipindi cha miezi iliopita baada ya kashfa ya unyanyasaji wa
kijinsia katika eneo la Rotherham na mauji ya mateka wa Uingereza
yaliofanywa na kundi la Isis.Facebook imesema kuwa iliamua kuzingatia usawa kati ya uhuru wa kujieleza na kuimarisha mazingira yalio salama,lakini pia ikasema kuwa haitakubali kuchapisha jumbe zinazowaingilia watu wengine kutokana na rangi au dini.
Twitter kwa upande wake imesema kuwa inazipitia jumbe zote zinazokiuka sheria zake zinakataa matamshi yoyote yanayoweza kuzua vurugu.
CHANZO BBC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni