Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Jumatano, 7 Januari 2015

ALSHABAAB LADAI KUWAUWA WAPELELEZI WA USA


Wapiganaji wa kundi la Alshabaab wamedai kuwaua wapelelezi wanne wa Marekani nchini Somali
Wapiganaji wa kundi la Alshabaab kutoka Somalia wanasema kuwa wamewaua watu wanne wanaodaiwa kuwa wapelelezi wa Marekani,Ethiopia na serikali ya Somalia.
Wanne hao wanadaiwa kupigwa risasi katika mji wa Baradhere siku ya jumanne baada ya jaji mmoja wa Alshabaab kuwapata na hatia ya kuwaunga mkono wapelelezi wa CIA na mashirika yanayokabiliana na kundi hilo.
Wiki iliopita maafisa wa Somali wanasema kuwa shambulizi moja la ndege lililotekelezwa na Marekani lilimuua kiongozi wa ujasusi wa Alshabaab Abdishakur Tahlil.
CHANZO BBC

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni