Huku ikiwa kutengeza mtoto ni swala
la furaha baina ya mke na mume,kujifungua ni uchungu ambao huwachiwa
mwanamke pekee. kulingana na vitabu vitukufu, uchungu unaohisiwa wakati
mwanamke anapojifungua ni laana na adhabu kwa wanawake kutoka kwa mungu
baada ya Hawa kumdanganya Adam kufanya dhambi na hivyo basi kumuasi.
Mbali
na kukaa katika chumba cha kujifungua wanaume wengi hupendelea kwenda
mbali ama hata kusafiri wanaposikia wake zao wanataka kujifungua.Hadithi kwamnba wanaume hutafuta sababu za kwenda mbali ama hata kujitafutia visafari zimehadithiwa wakati wake zao wanapokaribia kujifungua.
Baadhi ya sababu zinazotolewa na wanaume wakati huo ni kwamba hawawezi kukaa ndani ya chumba cha kujifungulia kwa kuwa kitendo hicho ni cha uchungu mwingi na kinatisha.
Je, unadhani wanaume wanafaa kuwa na wake zao wakati wanapijifungua?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni