Kansela Angela Merkel na viongozi wengine wakitoa salam za rambi rambi shambulizi la Ufaransa
Rais wa Ujerumani Joachim Gauck
amewahakikishia uvumilivu na ustahimilivu waislam million nne waliopo
nchini humo pamoja na tukio la shambulizi nchini Ufaransa.
Katika
kumbukumbu ya shambulio la mjini Paris Ufaransa mbele ya umati, Rais
Gauck alisema “sisi wote ni Wajerumani”. Amesema kuwa walitekeleza
shambulio Charlie Hebdo nia yao ni kutaka kuwagawa watu kwa matabaka ya
dini,lakini Ujerumani kamwe haiwezi kufuuata mgawanyiko huko kwa Waislam
waliopo Ujerumani. Awali viongozi wa kidini na kisiasa pamoja na
Kansela Angela Merkel walitoa salam zao za rambi rambi kwa kuweka maua
ubalozi wa Ufaransa nchini Ujerumani kama hatua ya kulaani shambulio
hilo.CHANZO BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni