Kikosi cha Yanga ya Dar es Salaam
Timu ya Yanga ya jijini Dar es
salaam hapo jana ilifanikiwa kutinga hatua ya Robo Fainali ya Mashindano
ya Kombe la Mapinduzi huko Visiwani Zanzibar baada ya kuitandika Polisi
ya Zanzibar mabao 4-0 kwenye Mechi ya Kundi A.
Ushindi huu ni wa
pili kwa Yanga kwenye Kundi lao baada ya kuichapa Taifa ya Jang’ombe
magoli 4-0 katika Mechi yao ya kwanza na sasa wanaongoza Kundi A wakiwa
na alama 6.Hadi Mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa mabao 2-0 ya Mchezaji wa Brazil Coutinho na yule wa Liberia Kpah Sherman.
Kipindi cha Pili Yanga walipiga Bao nyingine 2 kupitia Coutinho na Simon Msuva.
Katika Mechi nyingine zilizopigwa Jana Usiku, Azam FC iliichapa KMKM Bao 1-0 katika Mechi ya Kundi B na kupata ushindi wao wa kwanza baada ya kutoka 2-2 na KCCA ya Uganda katika Mechi yao ya kwanza.
Huku nao mabingwa wa kombe hilo Timu ya KCCA ya uganda wakifanikiwa kusonga mbele baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Timu ya Mtende ya Zanzibar
Mashindano hayo yanaendelea tena leo huko Visiwani Zanzibar kwa Mechi mbili katika uwanja wa Amani,Mechi ya kwanza ni kati ya Mtibwa Sugar na Mafunzo ikifuafuatiwa na mechi ya Simba dhidi ya Timu ya JKU.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni