Islamic State
Miili ya Watu zaidi ya 230
wanaoelezwa kuawa na Wanamgambo wa Islamic State imepatikana katika
kaburi la pamoja mashariki mwa Syria, Wanaharakati wameeleza.
Kaburi la pamoja liligunduliwa baada ya Watu wa jamii ya kabila la Sheitat kuruhusiwa na Viongozi wa Wanamgambo wa IS kurejea nyumbani.
Mwezi uliopita , Umoja wa Mataifa ulisema umepokea ripoti kuhusu mauaji mjini humo mwezi Agosti.
Wachunguzi wanasema kuwa inaonyesha kuwa mauaji hayo yalitekelezwa na wanamgambo wa Islamic State katika harakati ya kudhibiti rasilimali ya mafuta karibu na Mji wa Mohassan.
Mmoja kati ya manusura amesema aliona vichwa vingi vikiwa vimening'inizwa kwenye kuta, lakini yeye alifanikiwa kutoroka na familia yake.
Mauaji yanaripotiwa kutokea baada ya mazungumzo kati ya pande hizo mbili kuvunjika huku jamii ya kabila la Sheitat ikikataa kutekeleza yale waliyokubaliana na IS.
CHANZO BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni