Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Alhamisi, 18 Desemba 2014

BOKO HARAM TISHIO KWA WANAJESHI NIGERIA


Operesheni dhidi ya Wanamgambo wa Boko Haram imekuwa haizai matunda nchini Nigeria
Wanajeshi 54 wamehukumiwa adhabu ya kifo na mahakama ya Kijeshi nchini Nigeria kwa kukataa kupambana na Wanamgambo wa kiislamu, Boko Haram.
Wanajeshi walikutwa na hatia ya uasi ,kushambulia na uoga.Wanajeshi hao wanashutumiwa kukataa kupigana kurudisha miji mitatu iliyokuwa ikishikiliwa na Boko Haram mwezi Agosti.
Mwanasheria wa Wanajeshi hao amesema wamehukumiwa kifo cha kupigwa risasi na kikosi maalum huku Wanajeshi wengine watano wakiachiliwa.
Vikosi vya kijeshi vya Nigeria vimedai kuzidiwa silaha na Boko Haram, kwa kuwa hawapatiwi silaha za kutosha kupambana na Wanamgambo.
Boko Haram wanapambana kuunda himaya ya kiislamu kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
CHANZO BBC.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni