Rais wa Jakaya Kikwete
Waziri Mizengo Pinda amekatiza kwa
muda, ziara yake katika Falme za Kiarabu kwa maelezo kwamba ameitwa
nyumbani na Rais Jakaya Kikwete kwa shughuli maalumu.
Waziri Mkuu
ambaye yuko katika ziara ya kutembelea nchi za Falme za Kiarabu, ikiwa
ni sehemu ya kudumisha ushirikiano na kutafuta wawekezaji, amekatisha
ziara hiyo siku mbili baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji
Frederick Werema kujiuzulu kutokana na kashfa ya Escrow.Werema alijiuzulu juzi na Rais Kikwete akaridhia hatua hiyo, huku umma ukisubiri hatua zaidi dhidi ya mawaziri na watendaji wa Serikali waliotajwa katika sakata hilo.
Katika barua yake ya kujiuzulu, Jaji Werema alisema ushauri wake wa kisheria kuhusu Akaunti ya Tegeta Escrow haukueleweka na hivyo kuchafua hali ya hewa.
Kwa mujibu wa ratiba ya ziara hiyo, leo Waziri Mkuu alitarajiwa kufanya mazungumzo na washiriki wa maonyesho ya B2B pamoja na kutembelea maeneo mengine lakini ziara hiyo imefutwa na badala yake anaondoka asubuhi kurudi nyumbani.
Baadaye leo Pinda alitakiwa kwenda Doha, Qatar kwa ziara kama hiyo hadi Desemba 23.
Baada ya kukamilisha jukumu aliloitiwa, Waziri Mkuu anatarajiwa kurejea Falme za Kiarabu Jumamosi kuendelea na ziara yake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni