Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Jumatano, 17 Desemba 2014

MWANABLOGU ASHTAKIWA KWA KUMDHARAU RAIS.


Mtandao wa facebook.Mwanablogu wa kenya Robert Alai ameshtakiwa nchini Kenya kwa kutumia mtandao wa kijamii twitter Kumtusi rais.
Mwanablogu maarufu lakini anayezusha mzozo Kenya ameshtakiwa kwa kumdharau rais, kufuatia ujumbe alioandika kwenye mtandao wa kijamii twitter mapema wiki hii.
Robert Alai anashutumiwa kwa kumuita Uhuru Kenyatta rais ambaye haja komaa kupitia ukurasa wake wa twitter.
Amekana mashtaka na akaachiliwa kwa dhamana ya dola elfu mbili.
Robert Alai amekumbwa na mzozo mara kadhaa kutokana na anayoyaandika kwenye ukurasa wake wa twitter.
Miaka miwili iliyopita alikamatwa na kuhojiwa kwa kutuhumu kwamba msemaji wa serikali anapanga kumuua.
Leo amefikishwa mahakamani kukabiliwa na mashtaka ya kunuia kumtusi rais.
Waendesha mashtaka wameiambia mahakama kwamba huenda wakaongeza mashtaka dhidi yake punde uchunguzi utakapokamilika.
Wakili wake ambaye ni seneta maarufu Kenya, amepinga jaribio la serikali kumnyima dhamana.
Hakimu anayesikiliza kesi amemuamuru kutoandika ujumbe kama huo katika mitandao yote ya kijamii wakati uchunguzi na kesi dhidi yake inpoendelea.
Alai ana wafuasi zaidi ya laki moja kwenye ukurasa wake wa twitter, na anatambulika kwa kuwa mkosoaji mkali wa serikali.
CHANZO BBC.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni