Rais wa Baraza la Ulaya,Donald Tusk
Viongozi wa Ulaya wamemaliza kikao
chao mjini Brussels Ubelgiji, wakisema kwa sasa wameunga zaidi kuliko
ilivyokuwa katika kuikabili Urusi. Viongozi hao wameonyesha kuwa vikwazo
vya kiuchumi havitadhoofishwa licha ya matatizo ya kifedha
yanayoikabili Urusi. Badala yake hatua mpya za Umoja wa Ulaya zilizokuwa
zimewekwa kufuatia Urusi kulitwaa kimabavu jimbo la Crimea zimepitishwa
na zitaanza kutumika mwishoni mwa wiki hii
Rais mpya wa Baraza la
Ulaya, Donald Tusk akifunga kikao cha viongozi wa EU amesema Urusi na
vitendo vyake ni tatizo kubwa la kimkakati linaloikabili Ulaya.Bwana Tusk, waziri mkuu wa zamani wa Poland, aliongoza kikao cha wakuu wa karibu nchi zote ishirini na nane za Umoja wa Ulaya. Amesema vitendo vya Urusi ndani ya Ukraine na katika Ulaya ni changamoto na alibaini kwamba mataifa ya Umoja wa Ulaya yameungana zaidi kuliko ilivyowahi kuwa huko nyuma katika kukabiliana na Urusi.
Kwa hiyo Bwana Tusk ameonya kuwa Ulaya inahitaji mkakati wa muda mrefu wa aina yake,ambao si tu utakaoshughulikia matatizo katika wiki zijazo na miezi, bali miaka. Wakati huo huo viongozi wamekubaliana vikwazo vipya vinavyopiga marufuku uwekezaji katika jimbo la Crimea, ishara kwamba vikwazo hivyo havitalegezwa hadi Urusi itakapobadili msimamo wake kuhusu jimbo hilo.
CHANZO BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni