Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Jumatano, 17 Desemba 2014

TANZIA‬; AISHA MADINDA AFARIKI DUNIA!



Aliyekuwa mnenguaji wa bendi tofauti hapa nchini Tanzania Aisha Madinda afariki dunia na mwili wake wakutwa umehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala.
Mkurugenzi wa bendi ya Twanga Pepeta amesema kuwa alipewa taarifa na Daktari mmoja kuwa wameona kama mwili wa Aisha Madinda hospitalini hapo, ndipo akatuma watu kwenda kuangalia akiwemo Luiza Mbutu ili kuhakikisha kama kweli ni yeye ndipo walipogundua ni yeye.

“ Mimi nipo njiani natoka Kigoma kuja Dar es Salaam, ni habari ya kusikitisha sana maana Aisha amefariki katika mazingira ya kutatanisha sana, jana alikuwa mzima na anachati na watu kwenye simu leo napigiwa simu mwili wake umekutwa umehifadhiwa kwenye hospitali ya Mwananyamala, hata sielewi nini kimetokea”. Amesema Asha Baraka
Mungu ailaze roho ya Marehemu Aisha Madinda mahali pema peponi , Amina

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni