Wapiganaji wa Kurdi
Wapiganaji wa Kikurdi wamesema wamepeleka kikosi Kaskazini mwa Iraq ili kupambana na wapiganaji wa kundi la Islamic State IS.
Kikosi
cha Wakurd 8000 kilianzisha mashambulizi endelevu kuvunja zuio katika
mlima Sinjar ili kuwakomboa maelfu ya Wayazidi na watu wengine ambao
wamezuiwa huko na kundi la Islamic State.Operesheni hiyo imeanza jumatano wiki hii kwa ushirikiano na vikosi vya Marekani na wafuasi wanaunga mkono harakati hizo.
Jumla ya mashambulio 50 ya anga yamefanyika katika eneo hilo dhidi ya vikosi vya IS.
Mwandishi wa BBC aliyepo katika eneo hilo anasema wapiganaji wa Kikurdi wametumia nguvu kubwa ili kuhakikisha wanasonga mbele katika operesheni hiyo
chanzo bbc
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni