Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Ijumaa, 12 Desemba 2014

NI NANI MWANAMKE HUYU ALIYE ONEKANA AFGHANISTAN


Ni nadra kumuona mwanamke akiwa amevalia hivi mjini Kabul Afghanistan
Picha ya mwanamke akiwa amevalia nguo fupi sio kitu cha kushangaza katika miji mingi duniani.
Lakini picha ya hivi karbuni ya mwanamke akiwa amevalia nguo fupi imesambaza sana kwenye mitandao ya kijamii. Sababu kubwa? picha hii ni ya mwanamke akiwa mjini Kabul Afghanistan.
''Nilishtuka sana,''anasema mwanamume aliyeipiga picha hio, ambaye ni mwandishi wa habari mjini humo, Hayat Ensafi.
"Nilijua kama ilikuwa muhimu kutumia fursa hii kupiga picha hio, kwa sababu sijawahi kumuona mwanamke akiwa amevalia hivyo akitembea katika barabara za mji mkuu.
Wanawake wanakabiliwa na sheria kali kuhusu mavazi nchini Afghanistan. Baada ya kuipiga picha hio, Ensafi alijaribu kuongea na mwanamke huyo lakini alikuwa na haraka sana.
Baada ya Hayat kuiweka picha hio kwenye mtandao wa Facebook, maelfu ya watu walitoa maoni yao. Inaarifiwa watu wengi wamekuwa wakizungumzia picha hio sio tu kwa mitandao ya kijamii bali pia katika mitaa watu wanamzungumzia sana.
 Wanawake wengi huvalia mavazi ya kuficha nyuso na mwili wao mzima na wengi wamekerwa na mavazi ya mwanamke huyo
Baadhi ya watu kwenye Facebook wanasema kuna njama ya kisiasa hasa kwa yule aliyepiga picha hio.
''Ni mwili wake sio wako,'' alisema Siddiq. "Tunampongeza kwa ujasiri wake . Tunataka kuwoana wanawake wengi wakiwa wamejitokeza katika hali hio. ''
"Mwili wangu, haki yangu, .....sio kulazimishwa kuvaa hijab,'' aliandika mwanamke mwingine.
Baadhi walimkemea mwanamke huyo, wakisema'
"tunaishi katika nchi ya kiisilamu na hatuwezi kuruhusu watu kama mwanadada huyo katika taifa letu, '' aliandika Ahmad.
Mapema miaka ya sitini na sabini, wanawake nchini Afghanistan walivalia mabuibui na hata kujifunika nyuso zao lakini pia kulikwemo na wale waliovalia sketi fupi.
CHANZO BBC.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni